UTANGULIZI
Historia hii ya kabila la Waikizu ni sehemu tu ya utafiti uliofanywa na timu ya Bwana Mturi P. M. na kupelekea uchapishwaji wa kitabu cha "HISTORIA YA IKIZU NA SIZAKI", chapisho la Mwaka 2001. Utafiti huo ulijumuisha wazee mbalimbali ndani ya kabila la Waikizu na Wasizaki.
IKIZU NA WAIKIZU
Kabila la waikizu ni moja miongoni mwa makabila ya kibantu yanayopatikana nchini Tanzania. Kabila hili linapatikana mkoa wa Mara katika wilaya ya Bunda. Kwa asili "Waikizu" ambao ndio hasa wakazi ndani ya kabila hili la waikizu waliishi katika Utemi wa Ikizu ambayo kwa baadae ilibadilishwa na kuitwa tarafa ya Serengeti mara baada ya kuongezwa Utemi wa Sizaki. Dola ya Ikizu iko umbali wa Kilometa 56 mashariki mwa makao makuu ya mkoa wa Mara, Musoma; kilometa 24 kaskazini ya Bunda, mji mkuu wa wilaya.
Waikizu kwa asili ni wakulima na vile vile ni wafugaji wazuri, chakula chao kikuu ni ulezi, mihogo, mahindi, mtama na viazi vitamu. Chakula chao hasa tokea zamani kilikuwa ulezi, ingawa mihogo imejitokeza kuwa chakula chao kikuu kwa kipindi hiki huenda ni kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na ukame wa mara kwa mara. Lakini pia wakazi wa kabila hili hupendelea kulima zao la pamba kama zao la kibiashara.
Waikizu ni miongoni mwa makabila ya kibantu yaliyotokea kaskazini yapata karne ya 11. Kabila hili wana uhusiano wa karibu kitabia na kimila na kabila la Wagisu walioko Uganda na Wakisii waishio Kenya. Mkoani Mara wana uhusiano wa karibu sana Wasizaki ambavyo kwa hakika ni vigumu kuwatofautisha. Koo nyingi za Waikizu zimechanganyika na makabila ya Wasizaki, Wajita na Wazanaki.
Kabila hili la Waikizu lina mwelekeo wa kupenda maendeleo ya namna tofauti tofauti iwe ni ya mmoja mmoja au pamoja. Tokea awali wao ni rahisi sana kuiga taratibu nzuri za kimaendeleo kutoka kwa wageni.Maana imani yao kubwa ni kwamba ushirika wa pamoja katika maendeleo ndiyo nguzo ya ushindi. Mfano mzuri ni ule wa kabila la Mbilikimo waliotokea kaskazini na kujaribu kuvamia vijiji vya mashariki mwa dola ya Ikizu na misitu yake. Watu hawa walikuwa na lengo la kuangamiza koo zote ili wateke maeneo yao na kuyafanya kuwa milki yao. Lakini kwa bahati mbaya, mambo yalikuwa tofauti kwa watu hawa ambapo Waikizu wa ukanda huo mara tu baada ya kuingiliwa na mbilikimo hao waliunda umoja wao wa vijiji vitano: Kilinero, Kihumbu, Mariwanda, Bholaze na Bhotaza na wakauita "Shirika la Muriho"na wenyewe wakajiita "Abhamuriho" yaani wakiwa na maana kuwa "watu wa Muriho/wana-Muriho" jina ambalo bado lipo hadi hivi sasa. Kwa hakika muungano huu thabiti wenye nguvu na hari ya ukombozi uliwawezesha kuwashinda mbilikimo hao na kuwafukuzilia mbali kabisa mwa dola ya Ikizu na hata wakaelekea kusini mpaka kufikia misitu ya Zaire ambako ndiko makazi yao hadi hivi sasa.
Watemi wa dola ya Ikizu wakishirikiana na viongozi wazee wa kabila walianzisha taratibu nyingi zilizolenga ushirika wa pamoja katika kuinua maendeo. Vijana walipenda kusafiri kwenda sehemu nyingi wakichukua mifano ya kimaendeleo waliyoiona na kuja kuianzisha Ikizu. Mfano wa karibu ni ushirikiano aliouonyesha Mtemi Makongoro Matutu aliposhirikiana na wazee wa Kiikizu hata kufikia hatua ya kuanzisha shule za kwanza nchini zilizojulikana kama "Bush Schools". Shule ambazo baadae ziligeuzwa kuwa shule za msingi kamili. Bega kwa bega mtemi na wazee walianzisha ulimaji wa barabara kwa kujitolea ili kurahisha usafiri kati ya kijiji na kijiji. Walijichimbisha malambo katika sehemu kubwa ya dola hiyo ili kuondoa dhiki ya maji kwa watu na mifugo vile vile kwa njia ya kujitolea. Matokeo ya wingi wa maji watu wengi wa makabila mengine mbalimbali walihamia Ikizu na mifugo yao wakikimbia adha ya uhaba wa maji wakati wa kiangazi sehemu walizotoka. Malambo hayo yaliyochibwa baadhi bado yako yakitoa huduma kwa jamii zinazoishi sehemu hizi.
Chifu Makongoro akiwa ni mtu mwenye kipawa cha kuona mbali, akishauriana na wazee viongozi alitoa agizo sehemu ya Manyago kusijengwe chombo chochote cha dhehebu moja mpaka siku zitakapowadia pajengwe shule itakayojumuisha dini zote na makabila yote kwa faida ya Taifa zima. Matokeo ya ubashiri huo ulifanyika mwaka 1942, ukatimilika mnamo tarehe 8 ya mwezi wa 11 mwaka 1986 wakati ujenzi wa shule ya kwanza ya sekondari ulipoanzishwa Manyago, na tarehe 1 mwezi wa 3 ya mwaka 1987 Shule ya Sekondari Makongoro ilifunguliwa ikijumuisha dini zote na makabila yote. Shule hiyo ilipewa jina lake kwa heshima yake na kumbukumbu za jitihada zake za kupenda watu na maendeleo yao kwa ujumla.
1. Mke wa Kikombogere (i.e kabila lake)
2. Mke wa Kisukuma
3. Mke wa Kitaturu
4. Mke wa Kimasai
5. Mke wa Kikurya
6. Mke wa Kingoreme
7. Mke wa Kijita
8. Mke wa Kijaruo
Ili kuhakikisha kutakuwa na ulinzi na usalama katika miliki yake, hao wanawake aliwagawa katika makundi mawili kwa kufuata utaratibu alivyowaona kama ifuatavyo hapo chini:
a) - Mkombogere b) - Msukuma
- Mtaturu - Mmasai
- Mkurya - Mngoreme
- Mjita - Mjaruo
Katika kuzingatia utabiri wa babu zake alikotokea makundi mawili ya wanawake wake aliyafanya na kuyageuza kuwa kama vyama kamili vya kisiasa vinanyoangalia nchi kwa zamu ya miaka minane katika fani zote yaani kiutawala, kiuchumi, na kiutamaduni.
Kundi la mke mkubwa likaitwa Zoma, nalo likawa na makora yafuatayo:
1. Zoma
2. Ghibasa
3. Gini
4. Nyange
Kundi la pili yaani la mke wa pili likaitwa Saye, likawa na makora yafuatayo:
1. Saye
2. Nyambureti
3. Gamnyari
4. Mmena
Makora yote hayo manane kwa zamu ya kubadilishana ya miaka minane minane yaliongoza nchi kikamilifu. Yaliangalia usalama wa nchi, kama kuna hatariau adui, njaa au balaa lolote na ndiyo wenyewe wa kuamrisha mwenge (orokobha) utoke au msana upite nchi nzima kwa ajiri ya mvua. Pia walihusika na kufunga na kufungua njia.
Kama ilivyoelezwa hapo mbele kila Ikora toka upande mmoja huongoza nchi kwa miaka minane na hung'atuka na uongozi huenda upande wa pili kwa Ikora lenye zamu. Utaratibu wa kung'atuka utaelezwa baadae kinaganaga.
Muriho licha ya kuwa Mganga na Jemedari ilimbidi afuate unabii aliotabiriwa na manabii wa kwao Ikisu, huko Kenya-kuwa miliki yake aliyoiteka itapanuka sana, watu wengi watamtafuta wakitokea sehemu mbalimbaliza kigeni kuja kuwa raia wake, alianzisha nyumba (amaghiha) nane ambamo watapokelewa. Nazo alizipa majina kama ifuatavyo:-
1. Wazahya (Abhazahya)
2. Wamangi (Abhamangi)
3. Wasegwe (Abhasegwe)
4. Wamwanza (Abhamwanza)
5. Waraze (Abharaze)
6.Wahemba (Abhahemba)
7. Wagitiga (Abhagitiga)
8. Wazera (Abhazera)
Kila nyumba ina sehemu zinazoitwa koo au amaghiha kwa lugha ya kiikizu. Koo ni sehemu ndogo ya nyumba ambayo kila wakati yana panuka na kuwa kuwa hamati ya nyumba hiyo.
Jemedari Mriho, kabla ya kutoweka duniani kwa ajiri ya ulinzi na usalama aliigawa milki yake katika sehemu nne, kila sehemu chini ya mdhamini aliyemteua:-
1. Omuchero: Huyu alikuwa mkuu wa wote, alivaa jino la tembo (rikonge), alitembea na mkia mweupe na alikuwa mlezi wa nyumba zote nane alizoachiwa na chini ya udhamini wake.
2. Nyamau: Huyo alipewa kuangalia na kuongoza sehemu za Chamuriho i.e Mariwanda, Sarama A, Kilinero, Kihumbu mpaka milima ya Bhoraza na Bhotaza.
3. Sibera: Alipewa uongozi wa Nyamang'uta na sehemu za tambarare (i.e Kitang'anyi).
4. Chibhora: Huyo alipewa sehemu za Sizaki alizopelekwa hapo mbeleni kuzilinda baada ya vita ya pili dhidi ya mazimwi (Amanani).
Viongozi wote watatu; Nyamau, Sibera na Chibhora walikuwa walinzi na wadhamini wa amakora na orokobha, kila mmoja katika sehemu aliyokabidhiwa na jemedari Muriho.
Watu wengine walioachiwa wosia na jemedari Muriho ni kama wafuatao:-
Nyakishoko: Huyu inasemekana ya alikuwa binti wa Kishoko; kijana wa Muriho. Nyakishoko alipewa uwezo mkubwa na babu yake Muriho. Aliachwa Kilinero ikiwa ni kituo cha kupitia kwenda Chamriho kufanya mitambiko na utakaso. Yeye alikuwa na uwezo wa kuruhusu msafara kupita au kukataa kamwe usipite.
Wasato: Vile vile aliachwa Kilinero kama nabii na mganga wa nchi nzima.
Nyachamuriho: Huyu alipewa jukumu na baba yake la kupanua mipaka ya nchi na akahamia Meseze, Sarama Kati ya sasa na ndiye aliyeachiwa mawe ya mitambiko na utakaso wa baba yake.
Mwishowe, kabla hatujaingilia maingilio ya Nyakinywa na kundi lake inafaa tutaje mambo makuu ambayo yaliletwa na Muriho: Jemedari Muriho Nyikenge asili yake ni Ikisu Kenya, babu zake waganga na manabii walimtabiri atafika siku moja nchi moja yenye mlima mrefu atakuwa mkubwa wa nchi hiyo. Yeye mwenyewe pia alikuwa nabii na mganga.
Kiuchumi, Muriho na kundi lake walikuwa wakulima na ndio walileta mbegu za ulezi.
Kiutamaduni, kwa upande wa kuabudu, waliamini miungu wengi. Na Mriho alipotoweka bila kufa na kuzikwa inavyoaminiwa na wafuasi wake, walianza kuabudu mlima Chamriho, sehemu alizofikia kwa kuongoza na manabii na waganga ambao nimewataja hapo juu Nyakishoko, Wasato na waliofuatia baadae.
SURA YA KWANZA
HISTORIA YA MURIHO NYIKENGE
Kihistoria inasemekana ya kwamba mwanzilishi au Mwikizu wa kwanza kuingia sehemu hii ya Ikizu alikuwa shujaa mmoja aliyeitwa Muriho Nyikenge. Muriho yasemekana alitokea sehemu ya mbali Ukisu, Uganda na kuingia Ukisii katika Jamhuri ya Kenya. Tokea Kisii huyo kiongozi na kundi lake waliingia sehemu ya Ngoreme wakaingia kwa mzee mmoja aliyejulikana kwa jina la Magwesi. Hapo alipumzika kwa muda mfupi maana alikuwa safarini kaitafuata nchi aliyoahidiwa na wazazi na wazazi wake, yenye mlima mrefu nayo ikawa Ikizu. Alifika kwenye mlima ulioitwa Rosambisambi, ambao baadae ukaitwa Itongo Muriho.
Muriho mwenyewe alikuwa mganga wa na nabii na aliahidiwa na wazazi wake, ya kuwa atakuwa mtawala katika nchri yenye mlima mrefu na alijenga mji wake hapo hapo Itongo Muriho. Nia ya Muriho ilikuwa kwenda kwenye mlima Chamuriho, lakini hakufaulu mwanzoni, maana kulikuwa na watu wakiishi kando kando yake wa walioitwa Mbilikimo, yaani kwa lugha ya kiikizu walijulikana kama "Abhahengere" au "Nyawambonere". Muriho aliishi hapo na kundi lake huku akitafuta na kubuni mbinu za kuwaingilia hao Mbilikimo. Mbilikimo nao baadae waligundua kuwa kulikuwa na watu wakiishi hapo Rosambisambi. Hivyo waliondoka kwenda kuwashambulia lakini wanapofika hawaoni miji au watu kwa sababu Muriho alikuwa ameuzindika mji, ameuzungushia kitu kiitwacho "Orokobha" chenye uwezo wa kufanya adui asione chochote.
Muriho akaanza mbinu za kuwashambulia hao maadui. Kwanza akaenda mpaka kwenye mlima huo akazungusha orokobha chini ya mlima wote, na kuweka mizimu yake. Jumla ya mizimu na sifa zake ni kama ifutavyo hapa chini:
1. Mzimu wa kwa kwanza aliiuita Nyakame, maana yake ni ukungu na umande wenye baridi kama maji ya barafu kuwazuia Mbilikimo kuondoka mapema asubuhi.
2. Mzimu wa pili aliuita Chawasingi, yaani joka kubwa sana lenye jani (risingi) kichwani.
3. Mzimu wa tatu aliuita Mosanga, yaani nyoka yenye alama au kitu shingoni kinachowaka au kutoa mwanga kama nyota au tochi usiku.
4. Mzimu wa nne aliiuita Kebhorogota, yaani nyoka anayelia, nchi yote inatetemeka.
5.Mzimu wa tano aliiuita Itaho, yaani ni nyoka anayevuruga maji saa zote yanakuwa machafu kusudi adui zake Mbilikimo wasichote.
Mizimu yote mitano, kila mmoja aliuweka kwenye mto wake na kila mto ulijulikana kwa jina la nyoka aliyekuwemo humo mpaka siku hizi. Baada ya zindiko la mizimu kila kisima cha maji, maji yakawa machungu sana, hivyo Mbilikimowalishindwa kuyanywa. Mizimu nayo kwa upande wake ilikuwa kama silaha ya kuwashambulia adui zake ambao kwa wakati huo walikuwa ni Mbilikimo walipokosa maji na kwenda kwenye mito hiyo kujisaidia. Hivyo Mbilikimo walipokosa maji na kuogopa kuumwa na nyoka mitoni waliamua kuhama kutoka mlima Chamriho.
UHAMAJI WA MBILIKIMO
Mbilikimo walihama mlima Chamriho wakipitia njia ya Sarama "A", Gabarawe na kuendelea mpaka Mlima Rosori kwa kupitia Kongoro, wakipita kwenye mwamba uitwao Igonza na kuingia kwenye mto uitwao Nyitonyi. Na hapo wakaamua kuweka kambi yao kwenye mwamba uitwao "Nyabhahengere". Mwamba huo uliitwa hivyo kwa kuwa kilikuwa kituo cha cha kwanza baada ya kuuhama mlima Chamuriho.
Huko nyuma Muriho na kundi lake lililoitwa "Abhakombogere" waliwafuatia nyuma kila walimopita hao Mbilikimo na kuzindika kwa kupitisha orokobha mpaka mto Nyitonyi. Walipogundua Mbilikimo walikuwa wanaishi kwenye mwamba Nyabhahengere Mriho aliingia kwenye mto Nyitonyi akaweka madawa yake mtoni (amahika), maji yakawa machungu sana maadui wakashindwa kuyanywa hivyo wakaamua kuhama tena kwa sababu ya ukosefu wa maji ya kunywa. Walihama wakipitia njia ya Kehonda wakielekea mto Chamtigiti na kupitia kwenye nafasi ya mlima Chamhang'ana na kutelemka mpaka Hunyari, wakaingia katika mlima Wosanza na kukuta pango ambamo walianza kuishi wakitumia maji ya mto Chamtigiti Wibara. Mbilikimo walipohama kwenye mwambawa Nyabhahengere Muriho alizindika sehemu yote na kupitisha orokobha na kuwafuatilia mpaka kwenye pango la Wosanza wakaelekea kwenye milima ya Sizaki, wakaingia milima mmoja uitwao Barama na wakaingia pango liitwalo Kanyamwara. Mriho aliwatulia na kuendelea kuweka dawa zake kwenye maji na wakati huo huo hakusahau kuwa anapowafukuza kwenye pango kuweka dawa na kuzindika pango hilo ili wakitaka kurudi wawaipati sehemu hiyo tena.
Mbilikimo walihama pango la Kanyamwara na kuelekea sehemu za Kabasa na hatimaye kuingia katika pango la Nyaka na kufanya maskani yao ambayo tulivyokwisha kuona huwa ni ya muda tu. Mriho aliwafuatilia huku akiweka dawa kwenye maji na kuzindika sehemu yote hiyo kwa kupitisha orokobha. Mbilikimo walishindwa kuishi kwenye pango la Nyaka kwa kukosa maji. Hivyo walihama na kuekea ziwa Nyanza (i.e Victoria) ambako aliwasindikiza na kuwalaani wasirudi tena. Yasemekana hao hawakukaa ziwani ila walisambaa. Kundi moja lilivuka ziwa na kuelekea sehemu za mkoa wa sasa uitwao Kagera na kuingia msituni. Kundi jingine liliambaa kando ya ziwa mpaka kuingia katika mapori ya Tarime.
Mriho alipokwisha hakikisha kuwa maadui wa kwanza hawatarudi alirudi nyumbani kufanya mipango ya kuimarisha milki yake aliyojipatia. Alikwenda kwenye mlima Chamuriho kufanya utakaso, yaani ikimweso. Ikimweso ni sherehe ya kuzindua na kubariki kitendo cha kishujaa na cha ujasiri. Katika sherehe hizo Nabii na jemedari Mriho alizindua na kutakasa pango walimoishi Mbilikimo na kuhamisha mji wake toka mlima Rosambisambi mpaka ukawa kwenye hilo pango katika mlima Chamriho.
Baada ya vita hii ya kwanza Muriho alikwisha kuwa na watu wengi licha ya wafuasi wake na viongozi wake. Alijipatia wanawake wanane baada ya fanikio hilo aidha kwa kupewa aoe kama shukurani kwa unabii na uganga wake.
Mwishowe, Muriho Nyikenge kama kiongozi mkuu wa Ikizu na Sizaki alilazimika kupigana vita nyingine dhidi ya mijitu ya ajabu yaani mazimwi au kwa kilugha "amanani". Mazimwi au amanani yalikuwa yanaishi sehemu za Sizaki hata wakati Muriho anawafukuza Mbilikimo kupitia Sizaki mpaka Ziwa Nyanza. Yalikuwa mawindaji ya wanyama na watu kwa lugha nyingine walikuwa wanakula wanyama na watu. Kuondoa wasiwasi kwa watu wake na kutimiza utabiri aliopewa na babu zake ambao pia walikuwa waganga, aliamua kuyashambulia hayo mazimwi. Alitumia njia au mbinu zile zile za kuweka dawa kwenye maji, kuzindika na kuweka orokobha kila sehemu wanayoondoka adui kusudi wasiweze kurudi tena. Mazimwi hayo walikimbia mpaka Ziwa Nyanza na huku Muriho anayafukuza mpaka yakajitupa kwenye ziwa hilo na kutoweka kabisa. Wadadisi wa historia ya Ikizu na Waikizu mpaka sasa hawaelewi hao mazimwi yanaishi au yalihamia ulimwengu upi.
Wakati wa kurudi jemedari Murihoakiwa na kundi lake baada ya ushindi wa pili, Wasizaki walimwomba awalinde naye aliahidi kuwalinda akirudi nyumbani na kufanya utakaso. Sherehe ya utakaso, kuzindika na ikimweso zilifanyika sehemu hiyo na pia zilifanyika nyumbani kwake Chamriho. Na baada ya hapo Chibhora I alitumwa Sizaki kwenda kuilinda isishambuliwe na maadui kama alivyoahidi baba yake.
Baada ya ushindi wa vita zote mbili na kuweka ulinzi wa uhakika katika sehemu zote alizoteka , Muriho alianza kujenga nchi mpya itakayojulikana kama "Ikizu". Muriho wakati huo alikuwa kama nilivyoeleza awali ana wanawake wanane toka sehemu mbalimbali:2. Mzimu wa pili aliuita Chawasingi, yaani joka kubwa sana lenye jani (risingi) kichwani.
3. Mzimu wa tatu aliuita Mosanga, yaani nyoka yenye alama au kitu shingoni kinachowaka au kutoa mwanga kama nyota au tochi usiku.
4. Mzimu wa nne aliiuita Kebhorogota, yaani nyoka anayelia, nchi yote inatetemeka.
5.Mzimu wa tano aliiuita Itaho, yaani ni nyoka anayevuruga maji saa zote yanakuwa machafu kusudi adui zake Mbilikimo wasichote.
Mizimu yote mitano, kila mmoja aliuweka kwenye mto wake na kila mto ulijulikana kwa jina la nyoka aliyekuwemo humo mpaka siku hizi. Baada ya zindiko la mizimu kila kisima cha maji, maji yakawa machungu sana, hivyo Mbilikimowalishindwa kuyanywa. Mizimu nayo kwa upande wake ilikuwa kama silaha ya kuwashambulia adui zake ambao kwa wakati huo walikuwa ni Mbilikimo walipokosa maji na kwenda kwenye mito hiyo kujisaidia. Hivyo Mbilikimo walipokosa maji na kuogopa kuumwa na nyoka mitoni waliamua kuhama kutoka mlima Chamriho.
UHAMAJI WA MBILIKIMO
Mbilikimo walihama mlima Chamriho wakipitia njia ya Sarama "A", Gabarawe na kuendelea mpaka Mlima Rosori kwa kupitia Kongoro, wakipita kwenye mwamba uitwao Igonza na kuingia kwenye mto uitwao Nyitonyi. Na hapo wakaamua kuweka kambi yao kwenye mwamba uitwao "Nyabhahengere". Mwamba huo uliitwa hivyo kwa kuwa kilikuwa kituo cha cha kwanza baada ya kuuhama mlima Chamuriho.
Huko nyuma Muriho na kundi lake lililoitwa "Abhakombogere" waliwafuatia nyuma kila walimopita hao Mbilikimo na kuzindika kwa kupitisha orokobha mpaka mto Nyitonyi. Walipogundua Mbilikimo walikuwa wanaishi kwenye mwamba Nyabhahengere Mriho aliingia kwenye mto Nyitonyi akaweka madawa yake mtoni (amahika), maji yakawa machungu sana maadui wakashindwa kuyanywa hivyo wakaamua kuhama tena kwa sababu ya ukosefu wa maji ya kunywa. Walihama wakipitia njia ya Kehonda wakielekea mto Chamtigiti na kupitia kwenye nafasi ya mlima Chamhang'ana na kutelemka mpaka Hunyari, wakaingia katika mlima Wosanza na kukuta pango ambamo walianza kuishi wakitumia maji ya mto Chamtigiti Wibara. Mbilikimo walipohama kwenye mwambawa Nyabhahengere Muriho alizindika sehemu yote na kupitisha orokobha na kuwafuatilia mpaka kwenye pango la Wosanza wakaelekea kwenye milima ya Sizaki, wakaingia milima mmoja uitwao Barama na wakaingia pango liitwalo Kanyamwara. Mriho aliwatulia na kuendelea kuweka dawa zake kwenye maji na wakati huo huo hakusahau kuwa anapowafukuza kwenye pango kuweka dawa na kuzindika pango hilo ili wakitaka kurudi wawaipati sehemu hiyo tena.
Mbilikimo walihama pango la Kanyamwara na kuelekea sehemu za Kabasa na hatimaye kuingia katika pango la Nyaka na kufanya maskani yao ambayo tulivyokwisha kuona huwa ni ya muda tu. Mriho aliwafuatilia huku akiweka dawa kwenye maji na kuzindika sehemu yote hiyo kwa kupitisha orokobha. Mbilikimo walishindwa kuishi kwenye pango la Nyaka kwa kukosa maji. Hivyo walihama na kuekea ziwa Nyanza (i.e Victoria) ambako aliwasindikiza na kuwalaani wasirudi tena. Yasemekana hao hawakukaa ziwani ila walisambaa. Kundi moja lilivuka ziwa na kuelekea sehemu za mkoa wa sasa uitwao Kagera na kuingia msituni. Kundi jingine liliambaa kando ya ziwa mpaka kuingia katika mapori ya Tarime.
Mriho alipokwisha hakikisha kuwa maadui wa kwanza hawatarudi alirudi nyumbani kufanya mipango ya kuimarisha milki yake aliyojipatia. Alikwenda kwenye mlima Chamuriho kufanya utakaso, yaani ikimweso. Ikimweso ni sherehe ya kuzindua na kubariki kitendo cha kishujaa na cha ujasiri. Katika sherehe hizo Nabii na jemedari Mriho alizindua na kutakasa pango walimoishi Mbilikimo na kuhamisha mji wake toka mlima Rosambisambi mpaka ukawa kwenye hilo pango katika mlima Chamriho.
Baada ya vita hii ya kwanza Muriho alikwisha kuwa na watu wengi licha ya wafuasi wake na viongozi wake. Alijipatia wanawake wanane baada ya fanikio hilo aidha kwa kupewa aoe kama shukurani kwa unabii na uganga wake.
VITA YA PILI DHIDI YA MAZIMWI
Wakati wa kurudi jemedari Murihoakiwa na kundi lake baada ya ushindi wa pili, Wasizaki walimwomba awalinde naye aliahidi kuwalinda akirudi nyumbani na kufanya utakaso. Sherehe ya utakaso, kuzindika na ikimweso zilifanyika sehemu hiyo na pia zilifanyika nyumbani kwake Chamriho. Na baada ya hapo Chibhora I alitumwa Sizaki kwenda kuilinda isishambuliwe na maadui kama alivyoahidi baba yake.
JEMEDARI MURIHO AANZA KUJENGA MSINGI AU CHIMBUKO LA WAIKIZU
1. Mke wa Kikombogere (i.e kabila lake)
2. Mke wa Kisukuma
3. Mke wa Kitaturu
4. Mke wa Kimasai
5. Mke wa Kikurya
6. Mke wa Kingoreme
7. Mke wa Kijita
8. Mke wa Kijaruo
Ili kuhakikisha kutakuwa na ulinzi na usalama katika miliki yake, hao wanawake aliwagawa katika makundi mawili kwa kufuata utaratibu alivyowaona kama ifuatavyo hapo chini:
a) - Mkombogere b) - Msukuma
- Mtaturu - Mmasai
- Mkurya - Mngoreme
- Mjita - Mjaruo
Katika kuzingatia utabiri wa babu zake alikotokea makundi mawili ya wanawake wake aliyafanya na kuyageuza kuwa kama vyama kamili vya kisiasa vinanyoangalia nchi kwa zamu ya miaka minane katika fani zote yaani kiutawala, kiuchumi, na kiutamaduni.
Kundi la mke mkubwa likaitwa Zoma, nalo likawa na makora yafuatayo:
1. Zoma
2. Ghibasa
3. Gini
4. Nyange
Kundi la pili yaani la mke wa pili likaitwa Saye, likawa na makora yafuatayo:
1. Saye
2. Nyambureti
3. Gamnyari
4. Mmena
Makora yote hayo manane kwa zamu ya kubadilishana ya miaka minane minane yaliongoza nchi kikamilifu. Yaliangalia usalama wa nchi, kama kuna hatariau adui, njaa au balaa lolote na ndiyo wenyewe wa kuamrisha mwenge (orokobha) utoke au msana upite nchi nzima kwa ajiri ya mvua. Pia walihusika na kufunga na kufungua njia.
Kama ilivyoelezwa hapo mbele kila Ikora toka upande mmoja huongoza nchi kwa miaka minane na hung'atuka na uongozi huenda upande wa pili kwa Ikora lenye zamu. Utaratibu wa kung'atuka utaelezwa baadae kinaganaga.
Muriho licha ya kuwa Mganga na Jemedari ilimbidi afuate unabii aliotabiriwa na manabii wa kwao Ikisu, huko Kenya-kuwa miliki yake aliyoiteka itapanuka sana, watu wengi watamtafuta wakitokea sehemu mbalimbaliza kigeni kuja kuwa raia wake, alianzisha nyumba (amaghiha) nane ambamo watapokelewa. Nazo alizipa majina kama ifuatavyo:-
1. Wazahya (Abhazahya)
2. Wamangi (Abhamangi)
3. Wasegwe (Abhasegwe)
4. Wamwanza (Abhamwanza)
5. Waraze (Abharaze)
6.Wahemba (Abhahemba)
7. Wagitiga (Abhagitiga)
8. Wazera (Abhazera)
Kila nyumba ina sehemu zinazoitwa koo au amaghiha kwa lugha ya kiikizu. Koo ni sehemu ndogo ya nyumba ambayo kila wakati yana panuka na kuwa kuwa hamati ya nyumba hiyo.
Jemedari Mriho, kabla ya kutoweka duniani kwa ajiri ya ulinzi na usalama aliigawa milki yake katika sehemu nne, kila sehemu chini ya mdhamini aliyemteua:-
1. Omuchero: Huyu alikuwa mkuu wa wote, alivaa jino la tembo (rikonge), alitembea na mkia mweupe na alikuwa mlezi wa nyumba zote nane alizoachiwa na chini ya udhamini wake.
2. Nyamau: Huyo alipewa kuangalia na kuongoza sehemu za Chamuriho i.e Mariwanda, Sarama A, Kilinero, Kihumbu mpaka milima ya Bhoraza na Bhotaza.
3. Sibera: Alipewa uongozi wa Nyamang'uta na sehemu za tambarare (i.e Kitang'anyi).
4. Chibhora: Huyo alipewa sehemu za Sizaki alizopelekwa hapo mbeleni kuzilinda baada ya vita ya pili dhidi ya mazimwi (Amanani).
Viongozi wote watatu; Nyamau, Sibera na Chibhora walikuwa walinzi na wadhamini wa amakora na orokobha, kila mmoja katika sehemu aliyokabidhiwa na jemedari Muriho.
Watu wengine walioachiwa wosia na jemedari Muriho ni kama wafuatao:-
Nyakishoko: Huyu inasemekana ya alikuwa binti wa Kishoko; kijana wa Muriho. Nyakishoko alipewa uwezo mkubwa na babu yake Muriho. Aliachwa Kilinero ikiwa ni kituo cha kupitia kwenda Chamriho kufanya mitambiko na utakaso. Yeye alikuwa na uwezo wa kuruhusu msafara kupita au kukataa kamwe usipite.
Wasato: Vile vile aliachwa Kilinero kama nabii na mganga wa nchi nzima.
Nyachamuriho: Huyu alipewa jukumu na baba yake la kupanua mipaka ya nchi na akahamia Meseze, Sarama Kati ya sasa na ndiye aliyeachiwa mawe ya mitambiko na utakaso wa baba yake.
Mwishowe, kabla hatujaingilia maingilio ya Nyakinywa na kundi lake inafaa tutaje mambo makuu ambayo yaliletwa na Muriho: Jemedari Muriho Nyikenge asili yake ni Ikisu Kenya, babu zake waganga na manabii walimtabiri atafika siku moja nchi moja yenye mlima mrefu atakuwa mkubwa wa nchi hiyo. Yeye mwenyewe pia alikuwa nabii na mganga.
Kiuchumi, Muriho na kundi lake walikuwa wakulima na ndio walileta mbegu za ulezi.
Kiutamaduni, kwa upande wa kuabudu, waliamini miungu wengi. Na Mriho alipotoweka bila kufa na kuzikwa inavyoaminiwa na wafuasi wake, walianza kuabudu mlima Chamriho, sehemu alizofikia kwa kuongoza na manabii na waganga ambao nimewataja hapo juu Nyakishoko, Wasato na waliofuatia baadae.
II. CHIMBUKO LA WAIKIZU-NYAKINYWA
Historia ya Nyakinywa kama ilivyokuwa kwa Jemedari Muriho Nyikenge inaanzia mbali na vituko vingi ambavyo kwa njia fulani vyafanana na vya jemedari Muriho. Utangulizi wake, kwa upande mwingine ni tofauti kimsingi na kimtazamo.
Kihistoria inasemekana wazazi wa Nyakinywa walikuwa Wahima na wa ukoo wa kitawala huko sehemu za Uganda, Burundi, Karagwe na Geita. Baba yake Nyakinywa alikuwa mdogo wake mtemi mmoja wapo kati ya maeneo hayo yaliyotajwa. Mzee huyu alikuwa na Ng'ombe wengi sana. Siku moja kwa bahati mbaya ng'ombe wake mmoja alimeza hati za utawala (Ndezi) za kaka yake. Kaka yake alitaka ng'ombe huyo achinjwe ili hati hizo ziweze kuondolowa lakini mdogo wake alilipinga wazo hilo la ng'ombe wake kuchinjwa akiahidi kumtunza na kulisha vizuri ili akinya amrudishie kaka yake. Mtemi hakukubaliana na ombi hilo aliamuru ng'ombe huyo achinjwe na hati hizo ziondolewe na watumishi wake walifanya kadri ya amri ya mtemi alivyoagiza hivyo ng'ombe huyo alichinjwa na hati hizo zilitolewa na kukabidhiwa kwa mtemi. Kitendo hicho kilimuudhi sana mdogo wake ambaye aliamua kuhama, alichukua ng'ombe wake karibu wote akaondoka na watu wake, akasafiri kupitia sehemu nyingi mpaka mwisho na pembeni mwa Usukuma, sehemu iitwayo kwa sasa Kanadi. Huko Kanadi akawa mtawala na nchi ikaneemeka ikawa na ng'ombe wengi na maziwa yakapatikana kwa kuzidi mahitaji. Yakawa yanamwaga ovyo mitoni. Mvua zilipokuwa zinanyesha maziwa hayo yalisafirishwa sehemu za mbali. Mtemi alipoona jambo hilo aliwakataza watu wake wasimwage maziwa mitoni, lakini hawakufuata ushauri wake. Maziwa yaliyokuwa yakimwagwa mitoni yalisafiri hata kufika Umasaini. Wamasai waliyafuatilia mpaka wakafika Kanadi. Ikazuka vita kubwa dhidi ya Wamasai, watu wengi walikufa na Wamasai walichukua ng'ombe wengi na kwenda nao Umasaini.
Hali ya Kanadi ikazidi kuwa ya wasiwasi, hali ya baba yake ikawa mbaya na alipokaribia kuaga dunia alimuita Nyakinywa na dada zake wawili, Wahunda na Wang'ombe awape wosia. Nyumba ya mama Nyakinywa ndiyo ilikuwa na haki kurithi utawala wa nchi, lakini haikuwa na mtoto wa kiume. Hivyo alibashiri fujo kutokea baada ya kufa kwaketoka kwa kaka zake Nyakinywa wa nyumba nyingine kutaka kuwaua ili wasitawale. Wosia wa baba yao hao wasichana watatu ulisema yeye akifa waondoke Kanadi wasifi mpaka nchi yenye mlima mrefu huko utawala wao unawasubiri. Akawatabiria jinsi watakavyosafiri na mambo yote yatakayowakuta njiani kabla ya kufika mwisho na pia ishara ya mwisho ya mwisho kuwajulisha wamefika safari yao. Mwisho akawaombea na kuwabariki hao wasichana watatu.
Siku chache baadae baba yao alifariki na wakamkalia na kumlilia kama kawaida ya Mtemi anapoaga dunia. Baada ya siku hizo za laziam Nyakinywa na dada zake wawili walichukua hati za utawala, wakatoroka Kanadi na kuanza safari ya mbali ya kufuata nchi ya mlima mrefu na pango la ahadi. Walipofika katikati ya mbuga ya Serengeti, sehemu iitwayo Sanagora walimwona mnyama anayefanana na ng'ombe akija mbiyo akitokea mashariki kuelekea magharibi. Alipowafikia karibu akaanguka nchini na akafa. Punde kidogo walimwona mwindaji akija akafika wakasalimiana naye na wakamwomba huyo mwindaji awapasulie huyo mnyama tumboni mwake, ya kwamba kuna hati zao wanataka wazichukue na kuwa nyama yote achukue. Hiyo ilikuwa mojawapo ya maagizo ya baba yao. Mwindaji huyo hakulikataa ombi lao, hivyo alimpasua huyo mnyama na humo tumboni walikuta vitu vyao vya utawala vifuatavyo:
i) Zimbura-Mawe ya mvua
ii) Ebherongo-alama avaazo mtemi mikononi na zingine za shingoni
iii) Rigashoda-Ushanga ishara ya amani ya mtawala
iv)Vitu vya usiri vinavyowekwa ndani ya ngoma ya utawala
v) Ekebamba-Chuma cha utawala.
Walipomaliza kuchukua vitu hivyo walimwomba awachunie ngozi na awashonee mifuko ya kubebea vitu hivyo. Alitimiza ombi hilo la wasichana, na hao wasichana waligana naye na mwindaji huyo wakaanza safari kuelekea Sizaki wakiwa na mifuko yao yenye hati za utawala ndani. Walipofika kwenye mlima Changuge hapo walikuta makazi ya mzee mmoja Mhemba aliyeitwa Samong'enya na walikaribishwa vizuri hapo na kupata hifadhi kwa ajiri ya pumziko kwa siku chache huku wakiwa katika mipango ya kuendelea na safari yao. Katika hizo siku chache walizopumzika mawe ya mvua yaliongezeka yakawa mengi yakawashinda kubeba. Hivyo ilibidi dada mkubwa Wahunda abaki hapo ayachunge. Nyakinywa na Wang'ombe wakiwa na mifuko yao waliendelea na safari yao kuelekea Hunyari. Walifika Hunyari sehemu iitwayo Chahingo, walipumzika kwa muda na bahati nzuri Wang'ombe aliyekuwamjamzito alijifungua vizuri na akmwomba dada yake amsubiri. Lakini Nyakinywa aliamua kuendelea na safari na kuahidi kumrudia baada ya kufika mwisho wa safari. Hivyo Wang'ombe alibaki Hunyari.
Nyakinywa alivuka Mto Nyambogo nakupanda milima ya Kihumbu na kuufikia Mlima Nyakinywa akapumzika kidogo, kisha akaendelea na safari yake mpaka mapango ya Gaka. Alipoingia katika pango la Gaka alikanyaga jabali humo ndani lilia kama ngoma na alipolipiga lilitoa sauti ya ngoma halisi. Hivyo akaelewa kabisa amefika mwisho wa safari yakeakatua mzigo wake kwenye makazi yake mapya aliyotabiriwa na baba yake. Kesho yake Nyakinywa alitoka nje ya pango lake akaanza kuchunguza mazingira yake kwa mbali aliona Moshi ulikuwa unatoka mlima Sombayo. Alizidi kuufutia, akavuka Mto Kibangi na kuingia Sombayo ndani ya pango. Punde akatokea mtu mmoja aitwaye mwenye pango hilo ambaye alikuwa wa ukoo wa Muriho. Samwongo alimuuliza mgeni wake alikuwa anatoka wapi. Nyakinywa alimjibu alikuwa anatoka kwake na kwamba alikuwa amefuata moto. Alimwomba waongozane akaone kwake pia . Waliondoka pamoja mpaka Gaka kwa Nyakinywa ambapo baada ya kufika na kuwepo na mazungumzo zaidi, Samwongo alimuomba Nyakinywa waoane. Lakini ombi hilo lilikataliwa badala yake waliishi kama wapenzi.
Watu hao wawili waliishi kila mmoja na utaalamu wake. Samwongo alifahamu siri ya kutengeneza na Nyakinywa alikuwa na maji, yaani alikuwa na utaalamu wa kuleta mvua. Kila mmoja alimwomba mwenzake amwonyeshe utaalamu wake lakini hawakukubaliana. Mambo yaliendelea kuwa hivyo mpaka siku moja Samwongo alikwenda kuwinda, Nyakinywa akaleta mvua kubwa ikamnyeshea mwenzake huko porini akalowa, huku nyumbani mwenzake alizima moto. Aliporudi amelowa sana alikuta moto umezimika pangoni Gaka. Kwa hiyo Samwongo alilazimika amuonyeshe mwenzake namna ya kupata moto. Alitoa kibao cha moto na kijiti chake akapekecha mpaka moto ukatokea hivyo ikawa tayari amemuonyesha Nyakinywa siri ya utengenezaji wa moto. Alimwomba mwenzake naye amuonyeshe siri ya mvua. Nyakinywa hakukataa ombi hilo ila alimwomba mwenzake kwanza amletee dada yake Wang'ombe toka Hunyari, kisha aende porini aue mnyama aitwaye pongo, amchune huko huko aje nyumbani na ngozi peke yake. Samwongo alitimiza yote hayo kama alivyoagizwa, kesho yake Samwongo aliagizwa atengeneze miti ya kuwambia ngozi hiyo na Samwongo akaitengeneza. Hivyo wakaondoka watu watatu, ngozi ya pongo na miti ya mubamba ngoma kuelekea dimbwi la Nyambogo. Walipofika pale Samwongo aliomba awambe ngozi hiyo juuya maji alijaribu akashindwa. Nyakinywa alijaribu naye ikakubali kukaa juu ya maji. Samwongo aliomba ajaribu mara ya pili na ilikataa pia. Wang'ombe aliombwa ajaribu, yeye alifanikiwa kuwamba ngozi hiyo kama dada yake Nyakinywa. Hivyo Samwongo akaambiwa ameshindwa mtihani hivyo hataoneshwa utaalamu wa kuleta mvua na wakarudi nyumbani Gaka. Wakipofika nyumbani mambo yakageuka yaani Samwongo aliambiwa aoe binti yao ambaye ni binti yake pia. Ingawa mwanzoni alikataa lakini baadae hakuwa na jinsi alikubali na alimuoa na akawa mkwirima wao na akalazimika kujenga nyumba ya ngoma za utawala hapo nyumbani kwao Gaka. Mwishoni wakamwambia waweke mipaka kati ya Muriho na Kitang'anyi. Samwongo hakukubaliana na hilo jambo kwa sababu alikuwa na wakubwa zake na ndugu wengine ambao kama ingetokea ilitakiwa ni lazima washiriki katika jambo kubwa namna hiyo la kugawana utawala wa nchi.

MKUTANO MKUU WA NYAKINYWA NA ABHAKOMBOGERE WA KUMKABIDHI UTAWALA WA NCHI
Baada ya Nyakinywa kutokubaliana kabisa na Samwongo jinsi ya kuigawa nchi na utawala wake ikabidi mkutano mkuu uitishwe toka sehemu kuu mbili zinazohusika kutoa uamuzi wake. Mkutano huo mkuu ulijumuisha makundi makuu mawili kama ifuatavyo:-
b) Nyamau
c) Sibera
d) Chibhora
b) Wahunda
c) Wang'ombe
Kwa ujumla baada ya majadiliano ilikubaliwa kumkaribisha Nyakinywa katika utawala kwa masharti fulani.
- Abhakombogere
b) Nyamau
c) Sibera
d) Chibhora
- Abharaze
b) Wahunda
c) Wang'ombe
Kwa ujumla baada ya majadiliano ilikubaliwa kumkaribisha Nyakinywa katika utawala kwa masharti fulani.
MASHARTI
i) Sharti la kwanza ilikuwa la kuleta mvua kuonyesha kweli anao uwezo huo. Nyakinywa alitimiza kwa kufanya mvua inyeshe sana nchi nzima.
ii) Nyakinywa na watu wake walitakiwa kushiriki "uchero". Nyakinywa aliomba kwa kuwa yeye alikuwa Mhima hivyo waungane pamoja na kufanya nyangi ya pamoja na ombi lake lilikubaliwa. Hivyo nyangi hiyo ya ilijumuisha pia makora manane ambayo ni sawa na nyumba nane au hamati nane. Hapo aliomba wagawane nyumba hizi sawa kwa sawa. Abhakombogere walikubaliana na ombi hilo ila wakaweka sharti ya kuwa waruhusiwe kuweka orokobha yaani dawa ya kuzindika nchi nzima hivyo Waraze walikubaliana na tamko hilo.
Abhakombogere pia walimpa Nyakinywa sharti la kuleta mvua nchi nzima ili azime moto wa zamani na waweze kuwasha mwenge au moto mpya. Nyakinywa alikubaliana na ombi hilo la kunyesha mvua "Omosamo" nchi nzima. Masharti yake yote lazima yafuatwe na baadae tutayaona masharti yake hayo aliyowapa. Kwa pamoja mwishoni waliazimia nchi nzima kuwa na makundi au mafiga ambayo yatahusika katika uongozi wa nchi.
Hivyo wakambogere na Waraze (Nyakinywa) wakaungana kuwa kitu kimoja Waikizu wa mwanzo. Nchi nzima ikagawanywa sehemu mbili kufuatana na mkataba wa mkutano mkuu uliotajwa na kuelezewa wa kugawana nyumba nane. Nyakinywa akachukua nne na Abhakombogere wakachukua nne.
Sehemu mbili za nchi zikaitwa Muriho na Kitang'anyi. Nyumba zenyewe zikawa kama ifuatavyo;-
1. Muriho-Nyumba za Nyakinywa zikawa Abharaze (Nyumba za)
a) Abharaze
b) Abhahemba
c) Abhagitiga
d) Abhazera
2. Kitang'anyi- Abhazahya (Nyumba za)
a) Abhazahya
b) Abhamangi
c) Abhasegwe (Abhamanzi/Abhamagenibe)
d) Abhamwanza
A. UPANDE WA ABHAZAHYA
1. Wamangi-Hao walitokea Busega-Usukumani wakaingia Misarwa Sarama na wakatambulika kwa jina la "Abhamangi".
2. Sinde na Nyawaminza- Hao walitoka Busegwe- Zanaki na kuingia Ketare. Sinde akawa Mzahya na Nyawaminza akajiunga na Wamangi.
3. Wamwanza-Hao wa kwanza walitoka Ikoma na kuingia Sarama, Kongoro na wengine walitokea Zanaki na kujiunga na wenzao wa kutokea Ikoma wote wakawa Wamwanza.
4. Waturi-Hawa walitokea Buzilayombo mpakani mwa Geita na Biharamulo na kuingia Ikizu-Sarama na walipofika wakajiunga na Megabe na Masase wakawa Wazahya.
5. Masase na Megabe- Masase alikuwa Mzahya na Megabe alikuwa mhunzi rafiki yake toka Ntuzu aliyehamia Bumangi wakawa Wahunzi wote na mwishowe wakarudi tena Ikizu na kujiunga na Wazahya.
B. UPANDE WA WARAZE (ABHARAZE)
1. Waraze-Hao walitoka Kanadi, yaani Nyakinywa na kundi lake.
2. Wahemba-Hao walitokea Nyarero Waasi (Abhaasi) au Ndorobo na sifa yao kubwa walikuwa ni wawindaji hodari sana. Jamii hii iilikuwa ni kundi kubwa lililosafiri umbali mrefu kwa pamoja na walipofika Mugeta wakagawanyika.
Kundi moja likavuka Mto Tirina na kwenda Nata na wengine wakaingia Mlima Kabohemba uliooko Sarama A. Wengine wakaendelea mpaka Hunyari.
Wengine walitoka Kenya wakiwa na viazi na mitumbwi wakiongozwa na Nyambobhe wakafikia Mozemanga na baada ya ugomvi mzito baina yao na Wamwanza walihamia Mumwaro na Muriho.
Kundi la tatu lilitokea Usukumani wakiwa na mbegu ya mtama na moto wakapitia Changuge, Ushashi na baadae wakajiunga na wenzao wa Ikizu.
3. Wagitiga (Abhagitiga)- Hao wakiongozwa na Chamtigiti walitokea Sonzo sehemu za Arusha na kupitia Ikoma hadi Ikizu. Walikuwa wafugaji wa kondoo na walikuja nambegu za kunde.
4. Wazera (Abhazera)- Hao pia walitokea sehemu za Sonzo Arusha na kupitia Ikoma hadi Ikizu. Jamii hii walikuwa mashuhuri sana katika shughuri ya ufugaji wa nyuki kwa mantiki hiyo miongoni mwa mizigo yao mikubwa waliyokuja nayo ilikuwa ni asali.
*******************************Itaendelea*****************************************Abhakombogere pia walimpa Nyakinywa sharti la kuleta mvua nchi nzima ili azime moto wa zamani na waweze kuwasha mwenge au moto mpya. Nyakinywa alikubaliana na ombi hilo la kunyesha mvua "Omosamo" nchi nzima. Masharti yake yote lazima yafuatwe na baadae tutayaona masharti yake hayo aliyowapa. Kwa pamoja mwishoni waliazimia nchi nzima kuwa na makundi au mafiga ambayo yatahusika katika uongozi wa nchi.
Hivyo wakambogere na Waraze (Nyakinywa) wakaungana kuwa kitu kimoja Waikizu wa mwanzo. Nchi nzima ikagawanywa sehemu mbili kufuatana na mkataba wa mkutano mkuu uliotajwa na kuelezewa wa kugawana nyumba nane. Nyakinywa akachukua nne na Abhakombogere wakachukua nne.
Sehemu mbili za nchi zikaitwa Muriho na Kitang'anyi. Nyumba zenyewe zikawa kama ifuatavyo;-
1. Muriho-Nyumba za Nyakinywa zikawa Abharaze (Nyumba za)
a) Abharaze
b) Abhahemba
c) Abhagitiga
d) Abhazera
2. Kitang'anyi- Abhazahya (Nyumba za)
a) Abhazahya
b) Abhamangi
c) Abhasegwe (Abhamanzi/Abhamagenibe)
d) Abhamwanza
IV. MAINGILIO YA WATU WENGINE ZAIDI
Baada ya nyumba nane kugawiwa sehemu mbili
watu wengi zaidi walizid kuingia toka sehemu mbalimbali na kujiunga aidha kwenye nyumba ya Abharaze au abhazahya. Yafuatayo ni maelekezo kwa kifupi kuhusu watu hao:A. UPANDE WA ABHAZAHYA
1. Wamangi-Hao walitokea Busega-Usukumani wakaingia Misarwa Sarama na wakatambulika kwa jina la "Abhamangi".
2. Sinde na Nyawaminza- Hao walitoka Busegwe- Zanaki na kuingia Ketare. Sinde akawa Mzahya na Nyawaminza akajiunga na Wamangi.
3. Wamwanza-Hao wa kwanza walitoka Ikoma na kuingia Sarama, Kongoro na wengine walitokea Zanaki na kujiunga na wenzao wa kutokea Ikoma wote wakawa Wamwanza.
4. Waturi-Hawa walitokea Buzilayombo mpakani mwa Geita na Biharamulo na kuingia Ikizu-Sarama na walipofika wakajiunga na Megabe na Masase wakawa Wazahya.
5. Masase na Megabe- Masase alikuwa Mzahya na Megabe alikuwa mhunzi rafiki yake toka Ntuzu aliyehamia Bumangi wakawa Wahunzi wote na mwishowe wakarudi tena Ikizu na kujiunga na Wazahya.
B. UPANDE WA WARAZE (ABHARAZE)
1. Waraze-Hao walitoka Kanadi, yaani Nyakinywa na kundi lake.
2. Wahemba-Hao walitokea Nyarero Waasi (Abhaasi) au Ndorobo na sifa yao kubwa walikuwa ni wawindaji hodari sana. Jamii hii iilikuwa ni kundi kubwa lililosafiri umbali mrefu kwa pamoja na walipofika Mugeta wakagawanyika.
Kundi moja likavuka Mto Tirina na kwenda Nata na wengine wakaingia Mlima Kabohemba uliooko Sarama A. Wengine wakaendelea mpaka Hunyari.
Wengine walitoka Kenya wakiwa na viazi na mitumbwi wakiongozwa na Nyambobhe wakafikia Mozemanga na baada ya ugomvi mzito baina yao na Wamwanza walihamia Mumwaro na Muriho.
Kundi la tatu lilitokea Usukumani wakiwa na mbegu ya mtama na moto wakapitia Changuge, Ushashi na baadae wakajiunga na wenzao wa Ikizu.
3. Wagitiga (Abhagitiga)- Hao wakiongozwa na Chamtigiti walitokea Sonzo sehemu za Arusha na kupitia Ikoma hadi Ikizu. Walikuwa wafugaji wa kondoo na walikuja nambegu za kunde.
4. Wazera (Abhazera)- Hao pia walitokea sehemu za Sonzo Arusha na kupitia Ikoma hadi Ikizu. Jamii hii walikuwa mashuhuri sana katika shughuri ya ufugaji wa nyuki kwa mantiki hiyo miongoni mwa mizigo yao mikubwa waliyokuja nayo ilikuwa ni asali.
REJEA
Mturi, P. M (2001). Historia ya Ikizu na Sizaki. Goshen College Printing Service. Goshen-Indiana,
USA.
Huyo mke wa Kisukuma ndo aliitwa Nyakinywa Mtengeneza Mvua? Maana niko kutafuta ndugu zangu kutokana huyo, niliambiwa kuwa alikuwa kaka zake wawili Ganja na Nkhilomela ambao walikimbia baada ya tishio la kuuawa na baadhi ya waikizu walioona kuwa Himaya yao haiwezi kutwaliwa na wageni. Ganja aliuawa mikima ya balili but Nkhilomela alikimbia mpaka usukumani. Mimi ni great grandson wa Nkhilomela.
JibuFutaHakika mpendwa Nyakinywa asili yake ni usukumani...nimefurahi pia kusikia kutoka kwako juu ya Ganja na hata Nkhilomela nadhani kupitia wewe tunaweza kupata mengi pia juu ya watu hawa na chimbuko hasa la Nyakinywa..naomba mawasiliano yako kama hautojali@Ng'hili Dickson
FutaMawasiliano yangu ni +447459668082
JibuFutad.nghily@gmail.com
Asante sana ndugu tutadumu kuwasiliana ili kuweza kupashana habari juu ya mengi ambayo huenda bado hajajulikana juu ya mtu huyu muhimu katika historia ya kabila la Waikizu..Nikutakie heri na fanaka katika kuupokea mwaka mpya 2018
FutaOzomirye Sana kotoha ubwerea bwekabira yeto mungu akosakirye Sana inye mkwaya mozokoro oketereja omang'asa
JibuFutaOzomilye sana mwanaweto Mukwaya Omozokolo wa Keteleja
FutaSi
JibuFutaNaam...Karibu
FutaSIBANGA KINANDA SIGARA:nimesoma vizuri Kwa umakini mkubwa historya nzuri Sana ila kuna mambo yanakosa Kama vile ISAMONGO,NYAKINYWE pia namna xilivyopatikana koo na utani kiti ya Abhiro Abhatu na Abhakihumbu pia kwa mila wakizu tunafanana na wakisii-kenya na wakinga uganda pia hapa kwetu tunafanana sana na wanatta kwa mila wazee wa Natta na Ikizu walikuwa wanashilikiana kwa karibu sana; Tulehamwe wayeka
JibuFutaAsante sana kwa mrejesho ndugu yangu Sibanga Kinanda Sigara (Umwana wa Yeka). Kwa upande wa historia ya Nyakinywa ipo kwenye makala ya historia ya Ikizu na Waikizu-sehemu ya pili ambayo unaweza kuipata kupitia link iliyopo mwanzo wa Blog mkono wa Kulia...ila pia kupitia maoni yako nikuahidi kuwa nitaziambatanisha pamoja sehemu ya Kwanza na Pili ili kuondoa usumbufu wa kuhamahama (Navigation). Sambamba na hilo nikushkuru pia kwa kutoa nyongeza nzuri ya vitu vinavyopaswa kufanyiwa kazi ili kushibisha makala yetu juu ya kabila hili adhimu la Waikizu. Nikuahidi pia ya kuwa kwakuwa yote yanayoelezwa katika makala hii ni matokeo ya utafiti hivyo nikuondoe shaka ya kuwa yote uliyoyapendekeza na kuonesha shauku ya dhati ya kutaka yaonekane kwenye makala yamepokelewa na yatafanyiwa utafiti wa kina na baada ya matokeo ya tafiti hizo majibu yataletwa kwenye kama makala hivyo endelea kutembelea jukwaa kwa kadri utakavyoweza. Ahsante sana mwanaweto
FutaKumbe kile kisima cha Sibera kilitokana na huyo Sibera mtawala wa Nyamang'uta. Nimefurahi sana kwa somo hili zuri la kabila yangu pendwa #ABHIKIZO
JibuFutaHakika mwanaweto...ndivyo ilivyo. Ahsante sana kwa mrejesho, karibu pia ufatilie sehemu ya pili na zaidi upate kufahamu mengi juu ya kabila letu adhimu la Waikizu maana Ikizu ina wenyewe na wenyewe ndo sisi (Mimi, wewe na yule).
FutaElia kesona zambere
FutaNaitwa Masenza Wibhayo kutoka sanzate samahani ningependa pia kupata ukweli na uharisia wa chimbuko la jina masenza ndani ya kabila letu kutoka kwako mtaalam.
JibuFutaAhsante sana ndugu yangu Masenza kwa ujumbe wako mzuri juu ya andiko hili linalotoa maarifa juu ya kabila la Waikizu na Ikizu kwa ujumla..kwa bahati mbaya sana andiko lililobeba utafiti huu kulingana na mwandishi Mturi (2001) limeonyesha orodha ya majina machache kama sampuli (sample) kwa kuwa kiini hasa cha utafiti wake hakikuwa kushughurika na maana ya majina yote ya Kiikizu na maana zake na miongoni mwa majina hayo jina Masenza halimo..kwa kuwa huu ni uchokozi tu wa kitaaluma ili kufungua milango kwa tafiti zaidi nadhani hata hili pendekezo lako la kuangalia majina mbalimbali ya Kiikizu na maana zake yaweza kuwa eneo zuri sana la kufanyia utafiti kwa watafiti chipukizi ahsante sana.
FutaAsante sana pia kwa majibu yako thabiti.
FutaShukrani sana bwana Masenza
Futa